Mume Mtarajiwa Asepa na Milioni 60 za Mchumba Wake Siku Chache Kabla ya Harusi


Mwanamke moja wa nchini Japan amebaki hoi akisaga meno na kulia baada ya kutapeliwa na Mume wake mtarajiwa pesa ambazo zinafikia sawa na dola 30000 (zaidi ya milioni 60 za Tanzania ambazo alimpa Mume mtarajiwa huyo aliyemlaghai kuwa ni Mwana Anga na kumuahidi kumuoa pindi atakaporejea kutoka safari yake ya angani.


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 65 alituma kiasi hicho cha fedha baada ya kuahidiwa ndoa na Mwanaume huyo ambaye alimwambia kuwa ana safari ya kwenda mwezini na pindi atakaporejea atarudisha kiasi hicho cha pesa na kufunga nae ndoa.


Wawili hao walifahamiana na kuanza mazungumzo kupitia mtandao wa Instagram mwezi Juni mwaka 2022 huku wasifu wa Mwanaume huyo ukijazwa na picha za kuvutia alizopiga akiwa angani jambo lililomuaminisha Mwanamke huyo kuwa ni kweli Mpenzi wake huyo mpya alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Kimataifa cha Anga.


Uhusiano wao kupitia mtandao wa Instagram ulizidi kuimarika hadi kupanga mikakati ya ndoa ambapo kabla ya ndoa ndipo mwanaume akaomba mkwanja huo ili kugharamia safari yake ya roketi ya kwenda angani hivyo akamtumia pesa hizo kwa awamu tano lakini baadaye akagundua kaingizwa cha kike na hayupo huyo Mwana Anga aliyekua anataka kumuoa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad