Mume wa VERA Sidika Afunguka "Nitampenda zaidi Licha ya Kuondoa Makalio ya Bandia"


Mwimbaji wa muziki toka Kenya, Brown Mauzo yeye kwake umbo la kuvunja chaga sio inshu, ameeleza kwamba atampenda zaidi mke wake Vera Sidika na muonekano huu alionao hivi sasa tofauti na mwanzo.


@brownmauzo254 amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku moja imepita baada ya mkewe Vera Sidika kuweka wazi kufanyiwa upasuaji na kupunguza sehemu kubwa ya makalio yake baada ya kuona anapata matatizo ya kiafya.


Wawili hao ambao ni wazazi kwa mtoto mmoja wa kike, jina Asia, walikuwa pamoja katika mchakato wa upasuaji mpaka kukamilika. Brown Ameeleza. Pia amedai kulimiss umbo la awali la mkewe ila anachokipenda kutoka kwa Vera ni moyo wake.


Aidha, @queenveebosset yeye kupitia ukurasa wake wa Instagram, amewashauri wadada ambao wanampango wa kuongeza sehemu zao za mwili basi wasifanye hivyo kwani itawaletea matatizo kwa siku za usoni. Pia ameahidi kuonyesha video za tukio zima la kufanyiwa upasuaji wake.


✍️: @omaryramsey

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad