Mwanadada Awaongeza Wapenzi Wote wa Zamani Kwenye Kundi la WhatsApp Awatangazia Harusi yake




Mitandao ya kijamii katika kizazi cha sasa ni jukwaa bora la watu kujieleza kihisia na kimawazo pasi na kufungiwa na mtu yeyote.

Kijana mmoja kupitia ukurasa wa Tweeter ameweka woga wake pembeni na kufunguka jinsi alivyobwagwa na msichana aliyekuwa mpenzi wake.


Jamaa huyo mtumizi wa Tweeter kwa jina Prince Mudi alieleza kwamba kabla ya kupigwa buti, mwanadada huyo aliunda kundi kwenye mtandao wa WhatsApp kisha kuwaunga wanaume wote ambao walikuwa wamechumbiana naye, Mudi akiwa mmoja wao.

Mudi alieleza kwamab msichana huyo alikuwa na njama ya kutaka kuwakutanisha wanaume wote ambao wamewahi kuwa nao kimapenzi na baada ya kuwakutanisha kwenye kundi la WhatsApp, aliwapa taarifa kwamba anaolewa kisha akajiondoa kwenye kundi hilo na kuwaacha vijana wa watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue la kufanys, mwanzo hawajuani wala hawajawahi kuonana uso kwa uso!

“Mwaka 2017 nilichumbiana na msichana huyu kwa mwaka mmoja. Usiku mmoja aliniongeza kwenye kikundi cha WhatsApp bila mpangilio na akasema "nyote ni watu ambao sikuwataka na yamekwisha kwa sababu nitafunga ndoa wikendi ijayo." Alitoka mara moja na kutuacha tufahamiane,” Prince Mudi aliandika.


Wanamitandao hawakuweza kujizuia kutoa maoni yao kuhusu simulizi hilo ambalo lilionekana kama filamu ya kuigiza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad