Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 08/691 KJ Chandarua Mkoani Ruvuma, Sajenti Batsin Sanga amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwaua kwa risasi Mtalaka wake na Mwanajeshi mwenzake.
Ingawa jina la Askari aliyeuawa pamoja na Veronica halitajwi kwenye hukumu, ushahidi unaonesha Askari huyo alifyatua risasi 10 kati ya 30 alizokabidhiwa huku miili ya marehemu ikikutwa na majeraha ya risasi kichwani, hukumu imetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea, Yose Mlyambina aliyesema adhabu kwa anayepatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ni moja tu, nayo ni kunyongwa hadi kufa.