Mwimbaji wa Bongofleva @fobyofficial ameamua kutoa ufafanuzi juu ya kile alichokiandika jana kupitia insta story yake kumuhusu Hamisa Mobetto.
Foby leo ameamka na kusema kitendo alichokifanya jana cha kuhitaji yeye na Mobetto wamalize tofauti zao haiukuwa ni kuomba msamaha badala yake ni kuwa ameomba yaishe ili kuwepo na amani kati yao na pia sababu nyingine ni kuwa ame-mmiss msanii huyo.
Itakumbukwa, Foby jana alitumia insta story yake kumuangukia Mobetto na kuomba yaishe kwa kile alichoeleza kuwa ame-miss kuona picha zake baada ya kulambishwa block na mrembo huyo kwa takribani miaka 3 hii ni baada ya kutofautiana.