Tems ambaye jina lake halisi ni Temilade Openiyi, amewaambia mashabiki wa Kenya kupitia ukurasa wake wa Twitter hata yeye binafsi amesikitishwa na jambo hilo, anatazamia wakati mwingine kutua Kenya na kufanya onesho ambalo mashabiki wanastahili kupata.
Hata hivyo maelezo hayo ya Tems yanapishana na yale yaliyotolewa na waandaji wa tamasha la "Tukutane" (SIC) ambao wao kupitia taarifa yao waliyoitoa wameeleza kwamba, nyota huyo alishalipwa gharama zake zote siku 15 zilizopita, na tamasha lilikuwa lifanyike Oktoba 15.
Lakini ghafla meneja wa Tems akawaambia Tems hatoweza kuja kwenye onesho hilo, hajisikii kuja Kenya. Waandaaji wa "Tukutane", (SIC) wameeleza walishtushwa na taarifa hiyo iliyowavunja moyo. Aidha, wameomba radhi kwa mashabiki kufuatia kadhia hiyo na wanatazamia kupanga tarehe nyingine mpya kwa ajili ya tamasha hilo.
✍️: @omaryramsey