Mzee Aboubakar Said (64), mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza baada ya kumrubuni kwa kumpa shilingi elfu 10.
Kwa mujibu wa Eatv.tv. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Jackson Mwakagonda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho cha ukatili Oktoba 10, 2022 majira ya saa 8:00 mchana
Kaimu Kamanda Mwakagonda, amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikamatwa na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku akiwataka wazazi na walezi kuimariha ulinzi kwa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.