Nandy, Aggy Baby Wakubwa na Kesi Kama ya Zuchu, Kuiba Nyimbo


Leo hii Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bwana Ado November ameulizwa Kuhusu suala la Zuchu na Enock Jonas, amesema kwamba suala hilo limemfikia na jitihada za kutatua jambo hili zinaendelea.


Mbali na hayo Ado November amesema kwamba kupitia Enock kumshitaki Zuchu kumefanya Wasanii wengine kuja kwake na Kushitaki kwamba kuna wasanii wawili wameiga nyimbo yao bila Ruhusa yoyote.


Japokuwa Ado November hajawataja watu hao, lakini kwa upekenyuzi wangu najua kabisa hawa watakuwa ni Inafrika Band, maana ngoma yao "Indege" ndio imecopyiwa hivi karibuni na wanamuziki wawili, Nandy na Aggy Baby.


KWA MWENDO HUU MBONA WASANII WATANYOOKA, SASA INAFRIKA BAND WAKITAKA NA WAO MILLION 500, AGGY BABY ATAZITOA WAPI?

By Hopetyga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad