Nandy @officialnandy au Nandera; ni malkia wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, baada ya kuolewa na kujaaliwa mtoto mmoja wa kike kwa mumewe, Billnass au Nenga, kinachofuata ni madera tu na kusahau nguo fupi.
Nandy anasema kuwa, kwa sasa mashabiki wake wasitarajie kumuona kwenye vimini kwa sababu mumewe huyo amemkataza na yeye anatambua kabisa ni mke wa mtu.
Hayo yanakuja miezi mitatu baada ya kufunga ndoa yao ya kifahari ambayo iliweka rekodi itakayodumu hadi Novemba 19, mwaka huu kuona kama inaweza kuvunjwa na ile ya muigizaji Wolper anayokwenda kufunga na baba wa watoto wake, mfanyabiashara Rich Mitindo.