NETFLIX Yagoma Kuondoa Documentary ya Kanye West Kisa Maneno yake ya Kibaguzi Kwa Wayahudi


Kanye West alisema kuna influence kubwa sana ya wayahudi kwenye media na makampuni makubwa kwasababu ya uwekezaji wao na mara nyingi ni kandamizi, ila anafurahi kuona amegusa panapo wauma na siku zote yupo kwaajili ya kuongea ukweli. Hasa ukiachilia mbali makampuni mbali mbali ambayo yanaendelea kuachana na Ye, Netflix wao wamesimamia mlengo wao wa kibiashara, Kampuni hiyo ya kustream Movies imekataa kuiondoa kwenye mtandao huo documentary ya Kanye West inayoitwa Jeen-Yuhs.

Netflix wamedai Hakuna sababu ya wao kufanya hivyo, Documentary haina kauli za kibaguzi, hivyo hawawezi athiri project iliyopo kwenye mtandao wao kwa maneno ya kibaguzi ya mmiliki wa hiyo project, yaliyo ongelewa nje na utaratibu wao wa kazi. Mbali na hilo, Antonio Brown ametangaza kuendelea kuwa Rais wa Donda Sports, baada ya Aaron Donald na Jaylen Brown kuachana na Donda Sports.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad