Hii imetokea kwa baadhi ya Wazazi Wilayani Makete kuwaaminisha Watoto wao kuwa kufanya kwao vizuri kutawafanya Wazazi wafariki dunia kwa kuwa watashindwa kumudu gharama za kuwasomesha
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lupila, Tumwanukye Ngakonda amesema wamebaini hayo baada ya kuwahoji Wanafunzi wanaoelekea kuhitimu Elimu ya Msingi
Amesema wametoa elimu kwa Wanafunzi kutokubali kufeli na kuwaelezea umuhimu wa kufaulu mitihani hiyo