Mwanamuziki Nuh Mziwanda, leo, amefunguka na kusema anawashangaa wasanii wanaotoka kwenye lebo (usimamizi), wakati huko kuna afadhali kuliko kujisimamia mwenyewe.
@iam_mziwanda ameenda mbali zaidi na kusema kuwa ameshindwa hata kuachia EP (Extended Playlist) yake kutokana na kukosa usimamizi.
"Mimi nilitangaza kuachia EP ila mpaka sasa ishakua BP kwangu 😂 maana kila mtu ana mtu wake, Nawaonea huruma sana mnaotoka kwenye Usimamizi ðŸ˜" Ameandika @iam_mziwanda
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii mbalimbali kuvunja mkataba na lebo zilizokuwa zinawasimamia kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi hazijawekwa wazi.
Una mtazamo gani kuhusiana na hili, ni bora msanii kuwa chini ya usimamizi au kukomaa mwenyewe?