Wakati mashabiki wa Yanga wakiumizwa na matokeo ya sare nyumbani dhidi ya Al Hilal ya Sudan,takwimu zinaonyesha ni timu Moja pekee iliyoshinda kwake katika mechi katika mechi nne za jana.
Al Merreikh ya Sudan ndio timu pekee iliyoshinda nyumbani kwenye mechi za jana za mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakiifunga Al Ahly Tripoli ya Libya kwa mabao 2-0.
Yanga iko nyuma ya Al Merreikh ikiwa ni timu pekee iliyopata sare ya bao 1-1 Al Hilal wakichomoa,matokeo ambayo yamewachanganya mashabiki wao wakiilaumu timu yao.
Timu zingine tatu zilizopotoza nyumbani ni ASKO Kara ya Togo iliyopokea kipigo Cha mabao 2-1 dhidi ya JS Kabylie, ASN Nigelec ya Niger ilichapwa mabao 2-0 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.
Cape Town City ya Afrika Kusini nao wamepoteza nyumbani wakipigwa 3-0 dhidi ya Petro de Luanda ya Angola huku Leo kukiwa na mechi zingine 11 za hatua hiyo ya mtoano.
Timu zote zilizopoteza zina nafasi ya kubadili matokeo katika mechi za marudiano zitakazofanyika kati ya Oktoba 14-16.