Porojo za Oscar Baada ya Yangu Kushikwa Shati "Yanga haijawahi kuwa na uwekezaji mkubwa kuliko Al Hilal"


Matokeo kama haya yatawakomaza Wasemaji Vijana na kuwafanya kuwa na heshima dhidi ya timu Pinzani.

Yanga haijawahi kuwa na uwekezaji mkubwa kuliko Al Hilal. Yanga haijawahi kuwa na rekodi bora za CAF kuliko Al Hilal! Ni kweli Al Hilal misimu miwili iliyopita wamepungua ubora lakini sio wa kuwa wanyonge mbele ya Yanga!

Yanga anaweza kufuzu Ugenini lakini sio kwa Sababu ya uwekezaji wala wao kuwa Bora kuliko Al Hilal, HAPANA. Ni kwa sababu hata timu bora pia Duniani hufungwa. Ni kwa kuwa mpira sometimes unatupa matokeo tusiyotarajia.

Kusema utawapiga Al Hilal kama Ngoma, ni Disrespect! Udhaifu wao utauona sana wakicheza na timu Kama Mamelod, Raja Casablanca etc. Siku mbili hizi nimewacharura Yanga, sio kwa Ubaya. Wasemaji Vijana WALIWAJAZA sana utadhani Yanga wanayoisemea, ni tofauti na hii tunayoijua wote! Yanga bado haikupi uhakika wa Kimataifa, lakini ujenzi wa timu unaelekea kuzuri.

Yanga anaweza kwenda kufuzu ugenini lakini naamini kabla ya mechi hatuwezi kusikia tena kwamba “ Tutawapiga Kama Ngoma Khartoum” Wasemaji Vijana, wapunguze Mihemko, safari bado ndefu nimekaa paleeee!!!

Kuna Baba Mzungu mmoja tu Nchi hii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad