Rais Samia Suluhu Hassan ameteua wenyeviti wa bodi mbalimbali na watendaji katika taasisi mbalimbali hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 22, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa ameteua wenye viti wa bodi watano ambao ni Dkt. Florens Martin Turuka, Katibu Mkuu Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Aidha, amewateua Maofisa watano (05) kuwa Wajumbe wa Bodi ya DART kama ifuatavyo:-.Zainab Salome Msimbe, Mhasibu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;Mhandisi Johansen Jonathan Kahatano, Mkurugenzi wa Barabara, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA);
Bw. Aron Johnson Kisaka, Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Dodoma;
Pia amemteua Benjamini Kiloba Dotto, Mkurugenzi wa Miundombinu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA); na Bi. Mwantumu Mshirazi Salim, Katibu wa Kampuni, Export Processing Zone Authority (EPZA), Dar es Salaam.
Amemteua Beng’i Mazana Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.Beng’i ni Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Vilevile, amewateua Maafisa watano (05) kuwa Wajumbe wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:Dkt. Hemed Aziz Mpili, Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI);
Prof. Provident Jonas Dimoso, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Dodoma;Said Abdallah Panga, Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Dodoma;
Bw. Joseph Felix Chilambo, Meneja Uendeshaji Biashara, Benki ya Maendeleo ya TIB, Dar es Salaam; na Bw. John Mihayo Cheyo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais.
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2022.
Amemteua Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Mganga Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Prof. Nagu alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Tiba, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Prof. Nagu anachukua nafasi ya Dkt. Aifello Sichalwe ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi wa Prof. Nagu umeanza tarehe 19 Oktoba, 2022.
Aidha amemteua Bw. Deusdedit Kamalamo Bwoyo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii. Bw. Bwoyo alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki.
Uteuzi wa Bw. Bwoyo umeanza tarehe 20 Oktoba, 2022.
Amemteua Bw. James Mahanga Sando kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (Public Procurement Appeals Authority – PPAA). Bw. Sando alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Kampuni ya Crown Accounting and Consulting Firm, Dar es Salaam.
Uteuzi wa Bw. Sando umeanza tarehe 20 Oktoba, 2022