Rais wa Uganda Yoweri Museven Afunguka Kuhusu Mtoto wake kuwa Raisi wa Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema Wananchi wa Uganda ndio ambao wataamua kama Mtoto wake Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda anafaa kuwa Rais wa Nchi hiyo muda utakapofika ama laah!.


Kwenye mahojiano yake maalum na KTV, Museveni amesema kauli za Muhoozi anazoziandika Twitter haoni kama zitamsababisha asichaguliwe kuwa Kiongozi kwakuwa Viongozi wa Uganda hawachaguliwi Twitter.


“Viongozi wa Uganda hawachaguliwi Twitter, muda ukifika Wananchi watampima kuona kama anafaa na wakijiridhisha kuwa anafaa watafanya maamuzi”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad