RPC Simiyu Apata Ajali, Maswali Yaibuka Baada ya Aliyemgonga Kufariki




ACP Blasius Chatanda, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amepata ajali akiwa na gari lake binafsi T 462 BBD Toyata Harrier baada ya kugongwa na gari nyingine ndogo T. 766 CCZ Toyota Mark II lililokuwa linaendeshwa na Askari Polisi wa Wilaya ya Maswa F.5814 CPL Timoth Philipo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya kamanda huyo wa Polisi kwa waandishi wa habari, imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea Oktoba 02, 2022 katika mtaa wa Nyakabindi eneo la Mizani Barabara kuu ya Bariadi – Lamadi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari T 766 CCZ Toyota Mark II ambaye ni Askari Polisi, Badaa ya kuhama njia upande wake na kumfuata Dereva wa gari T 462 BBD Toyata Harrier ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa kisha kugongana uso kwa uso.

Kamanda huyo wa Polisi alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake pamoja na msaidizi wake PC Emmanuel, ikiwa pamoja na Askari Timoth ambapo walikimbizwa katika Hospitali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.


Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Askari Timoth Philipo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali Oktoba 03, 2022 alifariki baada ya sukari ya mwili kushuka na kushindwa kurudi kwenye hali yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad