Timu ya taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Girls imepata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya kombe la Dunia ya wasichana chini ya umri huo, fainali zinazoendela nchini India baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.
Mabao ya ushindi ya Tanzania yamefungwa na Diana Mnally amefunga bao la kwanza dakika ya 17 bao la pili limefungwa na Christer Bahera dakika ya 60 na lile la ufaransa limefungwa kwa mkwaju wa penati na Calba dakika ya 77
Kwa ushindi huu Serengeti Girls imefikisha alama 3 kwenye michezo miwili na wamepanda kutoka nafasi ya 4 hadi ya 2 kwenye msimamo wa kundi D.
Mchezo mwingine wa kundi hili unachezwa leo Saa 2:00 Usiku kati ya Japani dhidi ya Canada.