Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki


Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 ambalo Mwananchi imeliona imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).

Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999 ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.

Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.

Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.

Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000.

Via Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad