Baraza la Mitihani (NECTA) limekiri kupokea malalamiko ya Mwanafunzi aliyetoa malalamiko hayo na kueleza kuwa linafanyia kazi suala hilo kuhakikisha anapata haki yake
Mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim wa Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic alidai wakati akifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) Oktoba 5-6, 2022 alipangiwa namba 40 lakini jina lake lilikuwa namba 39 kwenye katarasi ya kusaini
Anasema alifanya mitihani 5 kwa namba 40 lakini mtihani wa 6 msimamizi akamwambia arudi kwenye namba yake ambayo ni 39, alipohoji kuhusu mabadiliko hayo Msimamizi alimjibu watalifikisha suala lake Baraza la Mitihani (NECTA)