Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini Jamaica, imefungia nyimbo zote zinazo hamasisha uhalifu, matumizi ya silaha na madawa ya kulevya ikiwemo Bangi ambayo ulimwa zaidi nchini humo.
Mamlaka hiyo imedai kuweka zuio hilo ni kuondoa fikra zilizo jengeka na wengi duniani kuwa uhalifu ni sifa inayokubalika nchini humo kama sehemu ya utamaduni wa jamii ya Jamaica.
Wasanii wengi nchini humo wakiwemo nguli wa muziki wa Reggae wamekosoa vikali katazo hilo na kudai haitasaidia kama serikali inavyo tazama, bali itaongeza zaidi uovu.