TCRA: Wanaotumiwa jumbe bila ridhaa toeni taarifa





MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi wanaotumiwa jumbe za maandishi na mitandao ya simu bila ridhaa yao watoe taarifa katika mamlaka hiyo, ili hatua za kisheria zichukuliwe. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari wakati ripoti ya utendaji wa sekta ya mawasiliano kwa waandishi wa habari kuhusu Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2022/23.

Dk Bakari alisema kitendo cha watoa huduma za simu kutumia wateja ujumbe bila ridhaa yao ni kosa la kisheria na kwamba wananchi wana haki ya kutoa taarifa TCRA ili hatua ziweze kuchukuliwa.

“Kama mtu hajaomba kutumiwa ujumbe wowote kutoka katika mitandao ya simu hilo ni kosa la kisheria na ana haki ya kutoa taarifa TCRA ili hatua nyingine ziweze kuendelea,” alisema.


Alisema mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu changamoto mbalimbali ambazo zinatokea kwenye huduma ya mawasiliano kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo aliwaasa watoa huduma kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na miongozi ambayo wameingia katika kutoa huduma zao.

Akizungumzia ripoti ya robo mwaka ya TCRA, DK Bakari alisema takwimu zinaonyesha mikoa mitano Tanzania inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika hadi Septemba 2022.

“Mkoa unaoongoza ni Dar es Salaam laini milioni 9.7, Mwanza milioni 3.7,  Arusha milioni 3.4, Mbeya million 3 na Tabora milioni 3., hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia  3.4 kwa laini za simu zinazotumika, ambapo hadi mwezi Juni 2022 kulikuwa na laini milioni 56.2 ila  hadi Septemba zilikuwa laini milioni milioni 58.1,” alisema.

Alisema idadi hii ya laini za simu inahusisha laini zinazotumiwa na watu na laini zinazotumiwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya mashine kwa mashine (M2M).

Mkurugenzi alisema uchambuzi wa laini hizo kwa watoa huduma unaonyesha kwamba kuna ushindani mkubwa; kwani hakuna mtoa huduma mwenye zaidi ya asilimia 35 ya laini zilizosajiliwa na kwamba mwelekeo wa usajili kwa miaka mitano iliyopita unaonyesha ongezeko la asilimia 8 kwa mwaka.

“Kuenea kwa laini miongoni mwa watu kumeongezeka kwa asilimia 4 kwa mwaka ambapo mwaka 2017 ilikuwa asilimia 78 mwaka 2018 asilimia 81, 2019 asilimia 88, 2020 na 2021 asilimia 91,” alisema.


Kuhusu gharama za vifurushi vya simu na data Bakari alisema wastani wa gharama za vifurushi vya simu zilikuwa Sh. 7.8 kwa kupiga simu ndani ya mtandao mwezi Septemba 2022, kutoka Sh. 7.7 Juni 2022 na wastani wa vifurushi vya simu kwenda mitandao mingine ulikuwa Sh. 8.1 Septemba 2022; ikiwa ni ongezeko kutoka Sh.7.6 Juni 2022.

Alisema wastani wa gharama za data Septemba 2022 zimebakia kuwa Sh. 1.8 kwa MB kama ilivyiokuwa Juni 2022.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Dk.Jabir Bakar
Aidha, Dk Bakari alisema watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.1 Juni  hadi milioni 31.1 Septemba 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.7, hivyo kuonesha ukuaji wa asilimia 17 katika kipindi cha miaka mitano.

Mkurugenzi huyo alisema idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii takwimu za ripoti hiyo ya utendaji wa sekta ya mawasiliano nchini zinabainisha mitandao mitano ya kijamii inayotumiwa zaidi, hivyo kuongoza kwa kiwango kikubwa cha data iliyotumika.

kwa kipimo

“Mtandao wa kijamii wa FaceBook uliongoza kwa kurekodi (GB Bilioni 2.59), YouTube (GB Bilioni 1.91), WhatsApp (Bilioni 1.58), na TikTok (GB Milioni 999) ikifuatiwa na mitandao mingine.

Dk Bakari alisema sekta ya utangazaji takwimu za utangazaji zinaonyesha kwamba zaidi ya visimbuzi milioni 3.3 vilikuwa hewani Septemba 2022 vikiongezeka kutoka milioni 3.1 Juni 2022 ambapo zaidi ya visimbuzi milioni 1.6 ni vya dijitali.

Aliitaja mikoa ya Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na visimbuzi zaidi ya milioni 1.2,  Arusha 272,702, Mwanza 261,237 na Mbeya 218,007 na Mikoa yenye visimbuzi vichache ni Songwe 1,568 na Katavi 16,990.

“Televisheni za waya (cable tv) zimeenea kutoka watu 16,786 waliounganishwa 2018 hadi 41,092 Septemba 2022.

Halikadhalika Dk Bakari alisema huduma za kifedha katika mtandao wa simu Tanzania inazidi kuendeleza mfumo jumuishi wa kifedha kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wanaofanya miamala kupitia simu za mkononi.


“Takwimu za mawasiliano za mwezi Septemba 2022 zinaonyesha kwamba huduma za pesa kupitia simu za mkononi zimeongezeka. Akaunti za pesa kwa simu za mkononi zineongezeka kutoka Sh.bilioni 38 Juni 2022 hadi Sh.bilioni 39.59 Septemba 2022.

Idadi ya miamala imeongezeka kutoka zaidi ya Sh.bilioni. 349.9 hadi Sh,bilioni 366.1 Septemba 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 katika miezi tisa,” alisema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad