Tiffah ni miongoni mwa watoto wa watu mashuhuri ambao wana wafuasi wengi kwenye mtandao wa instagram.
Muhtasari
Binti wa pekee wa staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz Tiffah Dangote ametia saini hati ya kusihi asiwe na mpenzi hadi atakapofikisha umri wa miaka 30.
Tiffah alionekana kwenye video akiwa na kaka zake ambao walitoa ahadi yake ya kutokuwa na mpenzi hadi 2045.
Alitia saini hati hiyo kabla ya kwenda kusalimiana na kaka zake kwa mtindo sawa na mikataba ya biashara
"Siamini ni ndugu zangu wanaonifanya nitie sahihi mkataba huu," Tiffah aliandika.
Mpango huo unakuja siku chache baada ya kumshangaza mamake Zari Hassan alipomwambia kuwa anataka kuwa video vixen na kucheza kama wanawake katika video za muziki za babake Diamond Platnumz.
Tiffah ni miongoni mwa watoto wa watu mashuhuri ambao wana wafuasi wengi kwenye mtandao wa instagram.