Tanzania (TRA) imewaonya wamiliki wa vyombo vya usafiri wanaotumia namba ambazo hazijatolewa na TRA ama Taasisi nyingine za Serikali ambazo zimepewa jukumu hilo kisheria.
Taarifa ya TRA kwenye mitandao ya kijamii imesema imebaini uwepo wa magari barabarani yaliyobandikwa namba kwa kutumia kwenye vibati ambavyo vina rangi tofauti na rangi zinazotolewa kisheria.
“Kumekuwepo na matumizi ya vibati vya namba vyenye rangi zisizotambulika kisheria vinavyowekwa mbele na nyuma ya vyombo vya moto, utengenezaji na matumizi ya vibati hivyo ni kosa kisheria kama inavyoelezwa kwenye Kifungu cha 8 cha Sheria ya Usalama Barabarani (The Road Traffic Act, 1973),”
TRA imesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote aatakayeendelea kukiuka sheria hiyo ikiwa ni pamoja na kutaifisha chombo cha moto husika.