Tundu Lissu Aiponda Ripoti ya Kikosi Kazi



Dar es Salaam. Makamamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema ripoti ya Kikosi Kazi iliyokabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni, imejaza upungufu na kwamba imeiga mambo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba.

Ameyasema hayo leo Oktoba 26 alipokuwa akichangia mjadala ulioandaliwa na Mwananchi Communications Lts kupitia Twitter Space, akisema ripoti hiyo imerudia makosa ya Katiba zilizotangulia kutegemea uamuzi wa Rais aliye madarakani.

“Taarifa hiyo inarudia kosa la tangu uhuru kuweka katiba mikononi mwa Rais, tangu mwaka 1962 katiba zetu zinalenga Rais anataka nini,” amesema Lissu.


Kuhusu mfumo wa uchaguzi, amesema ripotyi hiyo imependekeza mfumo uliofeli uliowahusisha watumishi wa Serikali kuwa wasimamizi wa uchaguzi.


 “Wamependekeza Tume iendelee kutumia watumishi wa umma kwenye uchaguzi, tangu mwaka 1995 hawa watumishi wa umma ni watu wa CCM, na kikosi kazi kinasisitiza waendelee kuwa wasimamizi,” amesema.


Kuhusu Katiba mpya amesema, “Kikosi kazi hakipendekezi kuwepo kwa katiba mpya kianapendekeza kuwepo kwa katiba ileile kwa kuipaka rangi,” amesema.


Hata hivyo, Lissu ameshauri kuwepo kwa mijadala ya kidemokrasia ili kufikia mwafaka wa kitaifa.


Mwananchi


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad