Baada ya Elon Musk kukamilisha ununuzi wa mtandao wa Twitter, ameanza kazi kwa kuondoa viongozi wajuu wanne (Top Executives) kwenye kampuni hiyo. Mkurugenzi mkuu wa Twitter Parag Agrawal na bosi wa fedha Ned Segal wameripotiwa kuondoka mara moja.
Mbali na hao, afisa mkuu wa sheria na sera wa kampuni hiyo, Vijaya Gadde naye pia ameripotiwa kuondoshwa na Mmiliki huyo mpya. Vijaya Gadde ndiye alimfungia Donald Trump kutumia mtandao huo.