Ukweli Kuhusu Mchezo wa Mieleka "Ni Maigizo Hakuna Ukweli"




Walio wengi wanafahamu mchezo wa mieleka na kuamini kuwa kila kitu ni cha kweli kwanzia yale mapambano hadi kutangazwa kwa mshindi wa pambano, lakini ukweli ni kwamba mchezo huo sio wa ukweli hauna uhalisia wowote na kilakitu huwa kimepangwa namna ya kufanyika ulingoni naweza sema ni maigizo yanayoendana na uhalisia.

Katika mchezo huo kabla ya wapambanaji kufika ulingoni hupangiwa sehemu ya kumpiga mwingine na namna ya kumrusha kama ambavyo hufanya, mshindi pia hupangwa kabla ya bambano kuwa fulani ndio anatakiwa kushinda.

Yote hayo ni kwajili ya kuburudisha watazamaji, wachezaji hutakiwa kuzingatia msingi ya mchezo huo mchezaji yeyote akivunja sheria kwa makusudi hulipa faini au adhabu ya kufungiwa mchezo.

Japo bahati mbaya hazikwepeki kwa wanaoumia hupata matibabu kutoka kwa madaktari wao, chakuelewa ni kwamba mieleka ni maigizo na sio uhalisia ndio maana wanasisitiza kuwa usijaribu ukiwa nyumbani kwakuwa ukifanya kwa uhalisia ni hatari.

Muanzilishi wa mchezo huo ni alikuwa Roderick James McMahons kutokea nchini Marekani , japo ukitaja mieleka (WWE) wengi hujenga picha ya wapambanaji maarufu kama vile John Cena,Undertaker,Ronda Rousey,Brock Lesnar na wengine wengi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad