Sasa Ukweli ni Kwamba Huyu Binti Anaye-trend mitandaoni ni Mdogo wake Mikala, tena Baba na Mama Mmoja.
Binti Huyo amefanya Interview na amefunguka mengi, kubwa zaidi amethibitisha kwamba Mikala hatupo nae tena, alifariki Mwaka 2009 kwa ajali mbaya huko Ughaibuni.
Binti huyo ameeleza kwamba Mara baada ya Mikala kuanza kuigiza Filamu wala wazazi wake hawakupenda afanye shughuli hiyo, hivyo ili kumuweka mbali na Bongo Movie wakaamua kumpeleka nje akasome.
Hivyo basi, huko Nje ndipo alipata ajali mbaya kiasi kwamba hata alikuwa hatambuliki, baada ya Ajali hiyo ya Gari, Baba yake aliitwa ili kupima DNA ndipo ukweli ukajulikana kwamba Katika Waliofariki kwenye Ajali hiyo na MIKALA YUPO.
Lakini Mbona Kuna baadhi ya Watu Wamewahi kufanyiwa Interview na wakafunguka kwamba Mikala yupo. Tumuamini yupi?
By Hopetyga