Umeshindwa kutoa wimbo kama 'Sukari', jaribu kuimba Chumvi - Zuchu akejeliwa Tweeter




Zuchu ashambuliwa Tweeter kwa kutoa ngoma zisizo ridhisha
Alhamisi mitandao ya kijamii haswa nchini Tanzania wamerauka kwa kumshambulia msanii Zuchu baada ya kutoa kibao kipya kwa jina KwiKwi.

Wengi waliomshambulia sababu zao ni kuwa msanii huyo hakufanya haki kutoa kibao hicho ambacho walikitaja kama kisicho na ladha hata kidogo.


Kupitia mtandao wa Tweeter, jamaa mmoja alimshambulia Zuchu kwa kusema kwamba msanii huyo kibao cha Sukari kilichovuma ndicho kibao pekee alichofanya haki na tangu hapo hajawahi toa kibao cha kuteka anga, licha ya kuachia vibao vingi tu.

Sanuka na Chapo kama alivyojiita mtumizi huyo wa Tweeter alimshambulia Zuchu kwa kusema kuwa bado ana deni kubwa sana kwa mashabiki wake kwani amekawia sana kuwatolea kibao cha kusisimua kama kile cha Sukari au hata kilichozidi kile.

Gumzo hilo liliibua utani mkali ambao wengine walisema kuwa kama Zuchu alitoa kibao cha Sukari kikawa kubwa na mashabiki wake wanasubiri kibao kikubwa zaidi kuliko Sukari basi ni heri msanii huyo atimbe studioni na kurekodi kibao cha Chumvi safari hii – huenda hicho kitamaliza deni na kusawazisha mambo.


“Zuchu Sukari inamtesa sana, ana deni la kutoa ngoma kubwa kuliko sukari,” Sanuka aliandika.

“Aimbe kuhusu chumvi sasa,” mmoja kwa jina Madenge alijibu kwa utani uliojawa kejeli.

“Umeandika utafikiri ana ugonjwa wa kisukari,” mwigizaji Idris Sultani alimjibu Sanuka.

Wengine walimtetea Zuchu kwa kusema kuwa kila msanii ana kile kibao ambacho kinakuwa cha moto zaidi hata kumshinda yeye mwenyewe kuachia kingine ambacho kinaweza ng’ata kwa makali zaidi yake.

“Ni kawaida lakini kwa msanii, kuwa na ile major hit ambayo kuifikia tena inakuaga kipengele kidogo. Ila Zuchu anauwashaaaa,” mmoja alimtetea Zuchu.

Mashambulizi haya si tu kwenye Tweeter bali hata kwenye mitandao yake mingine mashabiki walikejeli kibao chake kipya cha Kwikwi ambapo safari hii ilimlazimu Zuchu kuwajibu ili kuwatuliza.

“Napenda nyimbo zako sanaaa, lakini kwa hii kwikwikwi , inaudhi kusema kweli. Namaanisha ngoma ni mbaya nisiwe muongo. Usitoe hata video yake toa hit song ingine,” Mmoja wa mashabiki zake Instagram walimwambia ambapo Zuchu alimjibu kwa uchungu kuwa amemsikia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad