Mchosho wa Mtu kuwa mpweke, kutokuwa na furaha na kutokuwa na matumaini ya maisha kwenye utafiti huu kumeonesha kuongeza mpaka mwaka mmoja na miezi minane kwenye umri wa kawaida wa Binadamu na kuupita mchosho wa kuvuta sigara ambao humuongezea Binadamu mwaka mmoja na miezi mitatu kwenye umri wake.
Kudhoofika kwa mwili huongeza hatari ya kupata ugonjwa unaoathiri ubongo, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine mbalimbali ambapo Wataalamu wanaamini kutokuwa na furaha husababisha uharibifu wa seli na viungo muhimu vya mwili.
Watafiti wakiwemo wanasayansi kutokea Chuo Kikuu cha Stanford kilichopo nchini Marekani wamekadiria ni miaka mingapi iliongezwa kwenye maisha ya Mtu aliyeishi kwa upweke ambapo walitumia umri halisi wa Mtu pamoja na kupima damu, hali ya figo na BMI.
Utazeeka ukiwa na miaka mingapi ?