Utafiti waitaja Tanzania kuwa nchi ya pili kuamini ushirikina



Dodoma. Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili Afrika katika kuamini ushirikina ikitanguliwa na Cameroon kutokana na ukubwa wa matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina ikiwemo mauaji ya wazee 117 katika kipindi cha Julai 2017 hadi Mei 2018.Utafiti waitaja Tanzania kuwa nchi ya pili kuamini ushirikina

Mauaji hayo ambayo yalihusisha wanaume 91 na wanawake 26 yalifanyika katika kipindi hicho huku mkoa wa Tabora ukiongoza kwa kuwa na matukio mengi zaidi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Septemba 30, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha utafiti Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC), Fundikila Wazambi wakati akiwasilishaji mada kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Tanzania kwenye mkutano wa matokeo ya utafiti kuhusu kuchagiza haki za wazee.

“Kwa bahati mbaya Tabora ndiyo imeongoza katika takwimu za mauaji haya, ukiangalia vitendo vingi vya ukatili kwa kundi la wazee, wanawake, watoto hasa kubaka, kulawiti na mauaji vinasababishwa na imani za kishirikina. Utafiti uliofanyika unaonyesha Tanzania ni nchi ya pili kwa kuamini ushirikina ikitanguliwa na Cameroon,” amesema Wazambi.


Amesema lipo pia kundi la vijana ambalo halitaki kufanya kazi na badala yake wanatafuta njia za mkato kupata mafanikio.

Wazambi amesema kwa kipindi cha mwaka 2021 kumekuwa na matukio 155 yaliyoripotiwa kuvunjwa kwa haki za wazee na matukio 16 yaliyoripotiwa wazee kuvunjiwa haki kingono pamoja na kunyang’anywa mali, “Mwaka 2019 bibi wa miaka 77 alibakwa mpaka kufariki mkoani Dodoma.”

Akizungumzia masuala ya wazee katika vyombo vya habari na mtazamo wa jamii, Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Neville Meena amesema uzee umekuwa unapuuzwa na kudharauliwa kwa njia nyingi na unapigwa vita.


“Vyombo vya habari vinachangia ambavyo ni sehemu ya jamii. Vyombo vya habari vina wajibu wa kulilia kutungwa wa sheria kwani sera imekuwepo kwa miaka 20 sasa tuna wajibu wa kushawishi, tuonyeshe changamoto zinazoweza kuzibwa na uwepo wa sheria,” amesema Meena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad