Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo na kusema Serikali haiwezi kukaa kimya huku baadhi ya Watumishi wakifanya vitendo vya hovyo.
“Rais Samia Suluhu Hassan ameleta Tsh. Bilioni 7 za ujenzi wa Hospitali hii, fedha hizi za ujenzi ni lazima Wananchi waone thamani ya fedha za, siwezi kukubaliana na utendaji wa hovyo, fedha ziko hapa tangu Aprili, ni kwa nini hadi sasa majengo yapo kwenye linta? huu ni ubabaishaji”- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo Jumanne, Oktoba 18, 2022 wakati akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Migelegele mara baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma.
Kwa taarifa kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.