Wachezaji Young Africans waahidiwa NOTI Wakiifunga AL Hilal



RAIS wa klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said amewaahidi wachezaji wa timu hiyo kuwa watapata zawadi ya fedha endapo wataifunga Al Hilal katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza kufuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa.


Al Hilal itacheza dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Mkondo wa Kwanza kesho Jumamosi (Oktoba 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Akizungumza na Azam TV Hersi amesema, mchezo huo ni mgumu na muhimu kushinda kwa kuwa Young Africans ipo nyumbani, hivyo uongozi umeamua kuwaongezea ari wachezaji ili kupata ushindi.


Hata hivyo Hersi amesema kwa sasa hawezi kusema ni kiasi gani cha fedha ambacho watawapa wachezaji endapo watashinda mchezo huo lakini kitakuwa kikubwa.


“Hivi ni vitu vya kawaida na siyo mara ya kwanza kuwapa motisha wachezaji wetu pindi tunapokwenda kwenye mchezo muhimu kama wa Jumamosi. Kwa maandalizi yetu na ubora wa kikosi chetu naamini hiyo itakuwa kama mitisha kwao,” amesema Hersi.


Amesema malengo ya Young Africans ni kumaliza mchezo huo Dar es Salaam ili wawe na kazi ndogo watakapokwenda Sudan kwenye mchezo wa marudiano ambao ndio utatoa mshindi wa jumla.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad