Wakenya Wamvamia Mwanawe Museveni Jenerali Muhoozi Baada ya Kusema Naweza Kuipiga Nairobi Kwa Wiki Mbili



Mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba sasa anasema kuwa amewasamehe Wakenya ambao walimvamia kwenye mtandao wa Twitter.


Kupitia kwa ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Muhoozi ambaye ni kamanda wa jeshi nchini Uganda, anasema kuwa hana kinyongo licha ya kutukanwa akiahidi ushirikiano wa kuboresha kanda ya Afrika Mashariki.

“Wakenya kwenye mtandao wa Twitter, ninawasamehe kwa matusi yote mliyonirushia. Tafadhali tufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha Afrika Mashariki,” Muhoozi alisema.
Muhoozi avamiwa kwa kutuma jumbe za kivita akilenga jiji la Nairobi
Muhoozi aliwashangaza Wakenya baada ya kupachika jumbe za vita kwenye mitandao ya kijamii akilenga jini kuu la Kenya - Nairobi.

Muhoozi alidai kuwa kwa uwezo wake binafasi na ule wa jeshi la taifa la Uganda, kushambulia Nairobi na kuchukua udhibiti wake hawahitaji hata wiki mbili.


William Ruto Asukumiwa Presha Kuchukuwa Hatua Dhidi ya Mwanawe Museveni
“Haiwezi kutuchukua wiki mbili, mimi na jeshi langu, wiki mbili kuteka Nairobi. Ninafurahi kuwa wanachama wa wilaya yetu nchini Kenya wamejibu ujumbe wangu wa Twitter. Lakini bado ni wiki mbili kwa Nairobi,” Muhoozi alisema.
Wakenya hususan wale walio kwenye mitandao ya kijamii hawakufurahishwa na jumbe zake wakimvaa mzimamzima kiasi cha kukunja mkia na kusema amewasamehe.

Muhoozi ni kamanda wa vikosi vya ardhini vya jeshi la Uganda (UPDF) na babake alihudhuria uapisho wa Rais William Ruto mwezi jana ugani Kasarani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad