Wamuua baba yao kisha nao kuuawa



WATU wawili wanaosadikika ni majambazi, wameuawa na wanakijiji baada ya kumuua kwa kumkata mapanga Mzee Ephraim Mavika (57) wakimlazimisha kuonyesha fedha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi (ACP) Allan Bukumbi.
Watu hao wameuawa katika Kijiji cha Wasa Wilaya ya Iringa na katika tukio hilo, wanafamilia sita wamejeruhiwa na majambazi hao. Mmoja wa aliyeuawa ni mtoto wa marehemu Mavika.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi (ACP) Allan Bukumbi, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema tukio hilo lilitokea usiku baada ya vijana Matatizo Mavika na Christian Mavika kudaiwa kukodi majambazi kutoka  Mafinga wilayani Mufindi ili kutekeleza uvamizi huo.

Bukumbi alisema vijana hao walifanya uvamizi huo  baada ya kupokea taarifa zisizo sahihi kuwa Mzee Mavika ametumiwa kiasi kikubwa cha fedha na mtoto wake, Tedy Mavika, anayeishi Dar es Salaam.

Alisema  watu hao waliwavamia wanafamilia hao wakiwa na silaha za jadi zikiwamo mapanga na nondo.


Wakati  wa uvamizi huo, alisema  wanakijiji walipata taarifa na kwenda eneo la tukio na katika purukushani kati ya wavamizi hao na wanakijiji, wahalifu wawili kati ya saba walijeruhiwa na kufariki dunia.

Kamanda Bukumbi aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Matatizo Mavike, mkazi wa Wasa na Baraka Nyakunga ,dereva bodaboda mkazi wa mtaa wa Balali Mafinga, wilayani Mufundi.

Pia alisema watuhumiwa wawili ambao ni Hassan Mkalava, mkazi wa Ifunda na Christian Mavika, mkazi wa Ikugwe, Wasa, walikamatwa baada ya polisi kufanya msako na walipohojiwa walikiri kushiriki katika tukio hilo la uvamizi na mauaji.


Aidha, pikipiki mbili ambazo zilitumiwa na wahalifu hao zimekamatwa ambazo zina namba za usajili MC 578 DME rangi nyeusi na nyingine isiyokuwa na namba yenye injini namba KL162MJ rangi nyekundu zote ni aina ya King Lion.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad