Wasanii Cheed na Killy huenda kwa sasa wakawa hawataki kuona chochote kumuhusu Harmonize. Wawili hao wameamua kumpunguza boss wao huyo wa zamani katika kurasa zao za Instagram kwa kumu-unfollow.
Itakumbukwa, mapema wiki hii uongozi wa lebo ya Konde Music Worldwide ulitangaza kusitisha mkataba na wasanii Cheed na Killy kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi.
Aidha, wawili hao walifikisha malalamiko yao Baraza la Sanaa Taifa (Basata), na uongozi wa Konde Music uliitwa kwenye kikao kujadili kuhusiana na sakata la kuwatimua wasanii wao Killy na Cheed kwenye lebo yao.
Hata hivyo kikao hicho hakikuweza kufanyika kufuatia kile kilichoelezwa kwamba uongozi wa Konde Music Worldwide uliingia mitini baada ya kutakiwa kufika Basata.
Una lipi kwa wawili hawa? 🤔