Wema: Mama Whozu Amenikubali, Nimepitia Maisha ya Kusimangwa na Watu





Wema Isaac Sepetu au Tanzania Sweetheart; ni supastaa wa filamu nchini Tanzania ambaye kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kukubalika na mama mzazi wa mpenzi wake wa sasa ambaye Whozu.

 

Mara baada ya Wema kuthibitisha kuwa kwenye penzi zito na Whozu huku wakijiita Chimama na Chibaba, kuliibuka habari za mitandaoni kwamba familia ya Whozu akiwemo mama yake hawataki kabisa kusikia habari za mtoto wao kutoka kimapenzi na mlimbwende huyo.


Msanii Whozu.

Habari hizo zilidai kuwa, familia hiyo inamkubali mno video vixen Tunda ambaye amezaa na Whozu huku wakimuona Wema ni mkubwa kwa Whozu.

 

Hata hivyo, kupitia kipindi chake cha My Truth kinachrushwa kwenye Wemaapp, staa huyo anasema kuwa, mama Whozu anampenda na kumkubali kama ambavyo na yeye anampenda na kumkubali.

 

“Kitu kimoja ambacho naweza kukisema ni kwamba mama mkwe ninampenda na ananipenda hivyo tu,” anasema Wema na kuongeza;

 

“Nimepitia maisha mengi sana, nimepitia maisha ya kusimangwa, ikafika muda nikaona kama nimekata tamaa, lakini kwa sasa hivi sina msongo wa mawazo, mbona kwa sasa hivi nipo sawa sana?

 

“Sihitaji msaada wa mtu yeyote tena nasema sihitaji msaada wa mtu yeyote, kwa sasa nipo sawa sawia,” anasema Wema ambaye penzi lake na Whozu limekolea mno.

STORI NA SIFAEL PAUL |  GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad