WHO: CORONA BADO NI JANGA LA DHARURA DUNIANI



Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema janga la UVIKO-19 linasalia kuwa ni dharura ya ulimwengu ikiwa ni karibu miaka mitatu tangu lilipotangazwa mara ya kwanza kuwa janga.


Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Gebreyesus amesema katika miezi ya karibuni kwamba ingawa maambukizi yanapungua katika baadhi ya maeneo ulimwenguni, mataifa bado yanatakiwa kuendeleza umakini na kuwahimiza watu wao kupata chanjo.


Aidha amesema licha ya kushuka sana kwa idadi ya vifo tangu kuanza kwa janga hilo bado viko juu ikilinganishwa na vifo vilivyosababishwa na aina nyingine ya virusi. Kamati ya dharura ya WHO kwa mara ya kwanza ilitangaza UVIKO-19 janga la ulimwengu mnamo Januari 30, 2020.


Hatua kama hiyo husaidia kuharakisha utafiti, ufadhili na hatua za kimataifa za afya ya umma katika kudhibiti kusambaa kwa maradhi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad