WHO yaonya matumizi dawa nne za kunywa watoto barani Afrika



Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, Tedrso Adhanom Ghebreyesus AP - Salvatore Di Nolfi
Shirika la afya duniani, WHO, juma hili limetoa angalizo kuhusu matumizi ya dawa nne za kimiminika zinazotumiwa kutibu kikohozi na mafua, ambazo zinatengenezwa na kampuni kutoka nchini India, sharika hilo likisema zinahusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia.

WHO kwenye taarifa yake, imeongeza kuwa huenda dawa hizo ambazo zinatatizo, zikawa zimesambazwa nchi ya mataifa ya Afrika Magharibi, huku huenda ikawa imefika kwenye mataifa mengi ulimwenguni.

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, dawa hizo nne ambazo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara, zinaweza kuwa zilisababisha madhara kwa ini na vifo vya watoto 66.

Tedros, aliongeza kuwa “WHO inafanya kazi kwa karibu na kampuni zinazotengeneza dawa hizo pamoja na mamlaka za India”.


Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO, bidhaa hizo nne ni pamoja na Promethazine Oral Solution, Kofexmalin Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold Syrup.

Siku ya Alhamisi ya wiki hii, mamlaka nchini Gambia, zilikuwa zimeanza kukusanya dawa kadhaa za maumivu (Paracetamol) na promethazine syrup, kutoka katika maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Gambia, uchunguzi dhidi ya dawa hizi ambao ulianza mwezi Julai, bado unaendelea na kuongeza kuwa huenda bakteria aina ya E.Coli wakawa ni miongoni mwa sababu za kutokea mlipuko wa magonjwa ya figo.


Mamlaka za afya nchini Gambia, Septemba 23 mwaka huu ziliagiza kuondolewa sokoni kwa dawa zote za paracetamol na promethazine syrup.

Akizungumza akiwa mjini Geneva, mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, pia alionya kuhusu kuongezeka kwa magonjwa ya figo miongoni mwa watoto, akidai mpaka sasa kampuni zinazotengeneza dawa za kutibu bakteria E.Coli, hazijalihakikishia shirika hilo kuhusu usalama wake.

Tedros akisema miongoni mwa choo kikubwa cha watoto kilichopimwa, kilibainika kuwa na uwingi wa bakteria hao na tayari miongoni mwao walikuwa wametumia dawa ya kimiminika Paracetamol, akisisitiza kuwa dawa hizo zimebainika kuwa na kiwango cha juu cha diethylene glycol na ethylene glycol.

WHO inasema ripoti waliyopokea kutoka kwa taasisi ya udhibiti wa matumizi ya dawa za binadamu nchini India, ilionesha kuwa dawa hizo zilisambazwa nchini Gambia peke yake, lakini hata hivyo uuzwaji wa dawa hizo kwenye soko lisilo rasmi, huenda zikawa zimefika kwenye mataifa mengi duniani.


Shirika la afya sasa likizitaka nchi kushirikiana kuhakikisha wanaziondoa dawa hizo katika vituo vya afya na maghala ya kuhifadhi dawa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad