Yanga yajikita kileleni, yaichapa Geita Gold Kwao Kirumba



BAO pekee la mkwaju wa penalti ambalo limefungwa na Bernad Morrison katika dakika ya 45 limeihakikishia Yanga nafasi ya kuendelea kukaa kileleni mwa ligi huku ikiboresha rekodi ya kucheza michezo mingi bila kufungwa ikifikisha mechi 45.

Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ambao umeanza saa 10, ambapo ushindi huo unaifanya Yanga kuzidi kujikita kileleni ikifikisha pointi 20 na kumzidi mtani wao, Simba anayekamata nafasi ya tatu na alama 14.

Bao hilo pekee kwenye mchezo huo linepatikana katika dakika ya 45 baada ya Yanga kufanya shambulizi ambapo Heritier Makambo alipiga krosi ambayo imemgonga kwenye mikono mchezaji wa Geita Gold, George Wwa na mwamuzi, Florentino Zabroni kuamuru ipigwe penalti.

Baada ya maamuzi hayo, wachezaji wa Geita Gold walilalamika na kumzonga mwamuzi wakidai kuwa mwenzao alikuwa nje ya eneo la 18 (hakuwa ndani ya eneo la penalti) lakini mwamuzi akasiamamia msimamo wake huku akimuonyesha kadi ya njano, Masota na Danny Lyanga.


Ambapo Morrison amefunga mkwaju huo na kuipeleka Yanga mapumziko ikiwa kifua mbele, mchezo huo ulikuwa wa kuvutia na wenye ushindani kila timu ikitengeza mashambukizi huku kukiwa na kosa kosa kika upande.

Mabadiliko ya wachezaji ambayo yamefanywa kipindi cha pili yamenogesha mchezo huo na kuongeza ushindani zaidi ambapo Geita Gold iliwaingiza Offen Chikola, Miraji Athuman na Deus Edith Okoyo ikiwatoa Jofrey Manyasi, Raymond Masota na Juma Mahadhi.

Yanga iliwatoa Dickson Job, Denis Nkane, Haritier Makambo, Feisal Salum na Bernad Morrison nafasi zao zikizibwa na Yanick Bangala, Tuisila Kisinda, Fiston Mayele, Aziz Ki na Jesus Moloko.

Fiston Mayele nusura aipatie Yanga bao la pili mnamo dakika ya 73 baada ya kufumua shuti ambalo limeokolewa na kipa Arakaza McAthur na kuwa kona isiyo na faida, kipa huyo amekuwa nyota wa mchezo kwa upande wa Geita Gold akichomoa michomo mingi ambayo ilielekezwa langoni mwake.


YANGA: Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Ibrahim Bacca, Dickson Job/Yanick Bangala, Zawadi Mauya, Feisal Salum/Aziz Ki, Salum Abubakar 'Sureboy', Haritier Makambo/Mayele, Denis Nkane/Tuisila Kisinda na Bernad Morrison/ Moloko.

GEITA GOLD: Arakaza McArthur, George Wawa, Adeyum Salehe, Oscar Masai, Kelvin Yondani, Yusuph Kagoma, Raymond Masota/Miraji Athuman, Jofrey Manyac/Deusdedith Okoyo, Daniel Lyanga, Saido Ntibazonkiza na Juma Mahadhi/Offen Chikola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad