Young Africans kushirikiana na UNICEF, yasaini mkataba


Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans imesain
i Mkataba wa Ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto na Wanawake ‘UNICEF’, ambapo Mkataba huo utakuwa ni wa muda wa Miezi sita.


Mkataba huo wa Young Africans na UNICEF una lengo la kwenda kuhudumia jamii kwa kuhakikisha wanamichezo wanakuwa na afya njema (mashabiki) kwa kujikinga na magonjwa ya UVIKO-19 na Ebola.


Young Africans itakua na jukumu la kwenda kutoa elimu na misaada kwa jamii ya watu wenye mahitaji maalumu, na kwa wathirika wa magonjwa ya UVIKO-19 na Ebola.


Djuma Shabani alalamikiwa Young Africans

Kupitia Mkataba huyo, Klabu hiyo Kongwe Afrika Mashariki na Kati, inakwenda kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na magonjwa haya makubwa mawili kwa sasa.


“Gharama zote za kutekeleza mradi huu zinasimamiwa na UNICEF, kuna ada ambayo UNICEF inailipa Yanga katika kutekeleza miradi hii,”


“Tunashirikiana na UNICEF ili kila Mwanachama, Mpenzi na Mshabiki wa Young Africans na Vilabu vingine wapate maarifa na uelewa kuhusu chanjo ya UVIKO-19.


“Ni jukumu letu kama Klabu kuunga mkono juhudi zitakazotuwezesha kushinda UVIKO-19 na Ebola,”

“Tunajulikana kama timu ya Wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Wananchi,” amesema Rais wa Young Africans Hersi Said wakati wa kusaini mkataba huo


Naye mwakilishi wa UNICEF Fatimata Baladi amesema: “Young Africans imetuonyesha umuhimu wa michezo kwenye kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya ushirikiano wetu utasaidia zaidi ya mashabiki milioni 25 wa soka nchini Tanzania kupata taarifa sahihi kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na virusi vya Ebola ili waweze kujilinda.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad