MKUU WA Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Azam Fc Thabiti Zakaria maarufu Zaka Zakazi amefungiwa miezi mitatu na kupigwa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kuwatuhumu marefa kuwanyima penati mbili kwenye mchezo wa Prisons.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Azam FC kupoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa Sokoine Mbeya.
Taarifa hiyo imetolewa na Bodi ya Ligi Kuu baada ya kamati ya uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi kuu kukaa katika kikao chake Oktoba 4, 2022 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi hayo.
Aidha pia katika taaifa hiyo kamati haikuishia tu kumuhadhibu Zakaria bali pia klabu ya Namungo nayo imepigwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kuingia katika eneo la kiufundi la mchezo mara baada ya mchezo kumalizika.
Nayo Dodoma jijini imetozwa faini ya Sh500,000 kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka kwenye vyumba bya kubadirishia nguo jambo lililopelekea mchezo wao dhidi ya Simba kuchelewa kuanza kwa dakika moja