Zamalek yakataa kucheza Dar es salaam



Imefahamika kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Flambeau du Centre ya Burundi dhidi ya Mabingwa wa Misri Zamalek, hautapigwa tena Uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Uwanjani hapo kufuatia Mabingwa wa Burundi Flambeau du Centre kuuchagua Uwanja huo kama Uwanja wa nyumbani, kutokana na viwanja vya Bujumbura kukosa sifa ya kuhodhi michezo inayoratibiwa na ‘CAF’ na ‘FIFA’.

Mabadiliko hayo yemekuja baada ya Mabingwa wa Misri klabu ya Zamalek kulipa gharama za mchezo wa Mkondo wa Kwanza kushinikisha mchezo huo kupigwa mjini Cairo katika Uwanja wa Borg El Arab.

Inadwaiwa kuwa Zamalek imelazimika kuilipa Flambeau du Centre Dola za Kimarekani 50,000 (Sh 116milioni).


Hata hivyo mabingwa hao wa Burundi usingekuwa mchezo wao wa kwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex kwani mchezo wao dhidi ya Al Attihad ya Libya walicheza kwenye uwanja huo ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Taarifa kutoka ndani ya Zamalek zinasema kuwa wangetumia zaidi ya Dola 203,468 kama wangetua hapa nchini kwaajili ya mchezo huo wa mkondo wa kwanza.

Naye Rais wao Mortada Mansour amewapa wachezaji wa kikosi cha kwanza zaidi ya Dola Milioni Moja huku akitoa dola 407,000 kwa Wafanyakazi, Benchi la Ufundi na Wasimamizi wa klabu hiyo ili wagawiwe kabla ya mchezo huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad