ZARI MWILI UPO UZEENI, AKILI IPO UTOTONI



Wengi waliamini aliingia chaka la simba kwa Mondi. Siyo tu kwa hulka, hata kwa umri walipishana sana. Kilichopo kwenye ubongo wa Mondi, kilipita kwa Zari miaka mingi nyuma.


Kama ni u-VETA wa faragha. Zari alimaliza na neno "Asante". Mondi aliinuka kama katoka kunawa uso tu. Wapo walioamini hata watoto wale ni uzembe wa Dai na 'drai chama kituo'.


Lakini taratibu watu wakapata picha kuwa ukiachana na umri na utaifa. Pia makuzi yaalikuwa tofauti. Mondi ni mtoto wa kitaa, msela na mwenye njaa ya maisha. Zari alidata na 'taito'.


Kumiliki kiumbe kama Zari likawa zali kwake. Muda ulipoenda akazoea na kuanza kurudi kwenye asili yake. Ni baada ya kuona alichotaka ni kile kile. Akaanza kumpiga matukio.


Na 'laifu' la kiki za warembo kwake likaendelea. Hiki kitu ni kama ndoa ya Kikristu kwa Mondi. Hatoweza kuachana na kiki kwa pisi zake. Sasa ni Zuchu time!


Toka Sepenga na Penny na Mobetto hadi Zari. Raia wakaanza kumuonea huruma Zari. Kwa kuzama chaka la Simba toka Mbuga ya Tandale. Wakiamini hakustahili kutendwa.


Kosa la Zari halikuwa kumzalia Dai. Bali kutuama eneo lililomfaa Gigy na wenzake. Hizo ndo pisi zilizostahili kumiliki vurugu na hekaheka, za msela kichwa ngumu kama Mondi.


Umeona ya Zari huko insta? Na yeye kashindwa kuachana na maisha ya kumiliki vitoto. Anazeeka mwili, akili imebaki utotoni. Muda mwingi yupo 'bize' na kivulana umri wa mtoto wake.


Anajichetua kana kwamba anajibu pigo za Mondi na Zuchu. Ni kama gari limeweka ghafla, ana hekaheka kama kapandwa na siafu. Umri na kile afanyacho ni maji na mafuta.


Sijui ni Mondi aliyefanya ahusudu kuishi na vitoto. Au ndo 'fantas' yake.Kama taifa wifi tunaye. Tena wifi wa mwendokasi. Ana hekaheka huyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad