Aliyeishi Uwanja wa Ndege kwa Miaka 18 Aaga Dunia

 

Mtu mmoja raia wa Iran, Mehran Karimi Nasseri ambaye amekuwa akiishi katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris kwa miaka 18, amefariki dunia kwa mshituko wa moyo.



Nasseri, ambaye amefariki hapo jana Novemba 12, 2022 aliishi katika uwanja huo wa ndege kutoka mwaka 1988 baada ya kukosa hati za ukaazi na aliondoka Iran kwenda masomoni Uingereza mwaka 1974 na aliporudi alidai kufungwa kwa kumpinga Mfalme na kisha alifukuzwa bila ya pasipoti.



Kisa chake, kinaonesha kuwa aliomba hifadhi ya kisiasa katika nchi kadhaa barani Ulaya na baadaye Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, nchini Ubelgiji lilimpatia nyaraka za ukimbizi ambazo hata hivyo ziliibwa akiwa jijini Paris.


Kufuatia kadhia hiyo, Nasseri alikamatwa na Polisi wa Ufaransa lakini hawakuweza kumfukuza nchini humo kutokana na kutokuwa na hati rasmi za utambulisho wake na hadithi yake ikachangia utengenezaji wa filamu ya “The Terminal”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad