Ally Kamwe "Hatutaomba Ushauri Simba SC"



Afisa Habari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Ally Kamwe amesema kamwe klabu yao haitathubuti kuomba ushauri kwa watani zao Simba SC, ili ifanikiwe Kimataifa.


Wadau wengi wa Soka nchini Tanzania wamekua wakiushauri Uongozi wa Young Africans kuomba ushauri kwa wenzao wa Simba SC ili wafanikiwe Kimataifa, kutokana na klabu hiyo ya Msimbazi kuwa na mafanikio ya kufika Robo Fainali mara kadhaa kwa kipindi cha miaka mitano.


Kamwe amesema Young Africans haina uhusiano wa namna hiyo na Simba SC, zaidi ya kutambua wao ni klabu kubwa, yenye Wachezaji, Viongozi na Mashabiki bora nchini Tanzania, hivyo wanajua watafanya nini ili kufanikiwa Kimataifa.


Amesema ushauri wa Wadau wa Soka unaotolewa kuhusu kuomba ushauri kwa wenzao wa Simba SC wanauheshimu, lakini hawatathubutu kufanya hivyo.


“Sisi kama Young Africans kwanza hatuna mahusiano hayo na Simba SC, Kwanza tuwaombe Ushauri kwa lipi ‘ Sisi tuna Wachezaji wazuri tuna viongozi wazuri na tuna mashabiki Bora” amesema Ali Kamwe


Young Africans imekua ikihaha kurejea kwenye Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku mara ya mwisho kufikia mafanikio hayo ilikua msimu wa 1997/98.


Msimu huu 2022/23, Young Africans ilikaribia kuingia hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini ilishindwa kufuatia kufungwa na Al Hilal ya Sudan mabao 2-1.


Hata hivyo Klabu hiyo ina nafasi nyingine ya kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika, endapo itaifunga na kuitoa Club Africain ya Tunisia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad