Waafrika walianza kucheza soka tangu enzi na enzi. Wachezaji bora ambao dunia imewahi kuwashuhudia kama Didier Drogba, Jay Jay Okocha, Samuel Etoo, Yaya Toure na wengine lukuki ni baadhi ya waafrika . lakini kuna baadhi ya nyota wa kiafrika ambao walipewa uraia huko ugenini kwa ajili ya kucheza soka kwenye mataifa hayo na kulipa heshima bara la Afrika.
Wakati huohuo kuna wachezaji wengi wa Afrika wanaocheza soka la kulipwa kwenye ligi kubwa duniani kama English Premier League, Bundesliga, Serie A, League 1, na La Liga.
Ingekuaje siku moja kama nyota hao wote siku moja wangeamua kuru kucheza soka barani Afrika? Wangejiunga na vilabu gani vya Afrika?
Hapa kuna top 10 ya vilabu vya soka barani Afrika ambavyo kama nyota hao wanaocheza nje ya Afrika pengine wangependa kuvitumikia kama wangerejea kucheza soka kwenye ardhi ya bara la Afrika.
El Zamalek-Misri
Zamalek ni klabu ya mpira wa miguu inayopatikana Giza nchini Misri. Imeshinda mataji 22 ya kombe la Misri, mataji 11 ya kombe la ligi, kombe la klabu bingwa Afrika mara 5 na mataji 3 ya CAF Super Cup pamoja na African Cup Winners Cup.
Dynamos-Zimbabwe
Dynamos Football Club ilianzishwa mwaka 1963 baada ya miji ya Harare na Rhodesia kuungana. Tangu wakati huo wamehinda vikombe 15 vya Zimbabwe Premier Soccer League na vikombe 5 vya ligi.
Al Ahly-Misri
El Ahly ni neno linalomaanisha ‘Taifa’ kwa lugha ya Kiswahili. Klabu hiyo ya Misri ilianzishwa April 1907. Mwaka 2000 ilitangazwa na CAF kuwa klabu ya Karne kwa Afrika. Al Ahly ina jumla ya makombe 126, 19 kati ya hayo ni ya kimataifa na 109 ni ya ndani.
Makombe 19 ya kimataifa yanaifanya A Ahly kuwa ndiyo klabu yenye mafanikio zaidi duniani ikizipiku AC Milan na Boca Juniors.
Kaizer Chiefs-Afrika Kusini
Kaizer Chiefs inatumia uwanja wa Soccer City uliopo Soweto ambao pia unafahamika kwa jina la FNB Stadium.
Wameshindwa mara tatu ubingwa wa Premier Soccer League, wameshinda mara tatu ubingwa wa National Soccer Leagua na African Cup Winners mara moja.
AS Vita Club-Congo DR
Association Spotive Vita Club ni timu ya soka inayopatikana Kinshasa, klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1935 na kuanzia wakati huo imefanikiwa kutwaa mataji 12 ya Linafoot pamoja na mataji mengine 9 ya Coupe du Congo. Lakini pia wameshinda kombe la Challenge Papa Kalala mara mbili huku wakiwa wametwaa taji la klabu bingwa Afrika mwaka 1973.
Al Hilal Omdurman-Sudan
Hii ni klabu ya Sudan ambayo imeanzishwa February 1930 na makazi yake ni kwenye mji wa Omdurman. Wameshinda Sudan Premier League mara saba kwenye misimu 9 iliyopita pekee huku wakiwa wameshatwaa taji hilo mara 27 kwa ujumla.
Raja Casablanca-Morocco
Raja ilianzishwa mwaka 1949 na kwasasa ni klabu ambayo inafahamika zaidi nje ya mipaka ya Morocco. Mwaka 2000 ilichukua nafasi ya tatu kwenye orodha ya vilabu vilivyofanya vizuri kwenye mwongo uliopita kwa mujibu wa CAF. Raja imeshinda mataji 10 ndani ya Morocco.
Ilikuwa ni klabu ya kwanza kutoka Afrika kushiriki michuano ya FIFA World Club Championship mwaka 2000 nchini Brazil.
Esperance de Tunis-Tunisia
Eserance de Tunis ilianzishwa rasmi January 1919 wanacheza kwenye uwanja wa Stade Olimpique d’El Menzah. Eserance imeshinda mataji 26 ya ligi kuu ya Tunisia. Tunisian League Cup mara 14 na Tunisian Super Cup mara mbili.
Wameshinda CAF Champions League mara mbili, Arab Club Championships mara mbili na Arab Super Cup mara moja.
Al-Merrikh-Sudan
Hii ni klabu nyingine inayopatikana kwenye mji wa Omdurman, Sudan ambayo inatumia uwanja wa wake unaofahamika kwa jiana la Merrikh Stadium maarufu ka Red Castle. Klabu hii ni miongoni mwa klabu ngongwe barani Afrika imeshinda mataji 18 ya Sudan Premier League.
Al- Merrikh imeanzishwa mwaka 1908 na imekuwa klabu ya kwanza kushinda taji la Sudan football Championship mfululizo mwaka 1934.
TP Mazembe-Congo DR
Tout Puissant Mazembe (TP Mazembe) zamani ilifahamika kwa jina la Englebert inatajwa kuwa ndiyo klabu yenye mafanikio zaidi barani Afrika. Klabu hii ambayo inapatikana mjini Lumbumbashi huku ikitumia uwanja wake wa Stade TP Mazembe.
Mazembe ina pato la takribani Euro milioni 14 kwa mwaka kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato.