Auawa na Walinzi wa Shule ya Sekondari Kirumba, Familia Wagoma Kuzika Mwili




Familia ya kijana Ibrahimu Shakiru, inayoishi mtaa wa Kabuhoro B, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, imegoma kuuzika mwili wa kijana huyo kwa madai kuwa hadi haki itendeke kwa waliompiga hadi kupelekea kifo chake.
Kijana huyo alifariki dunia baada ya kupigwa na walinzi wa shule ya sekondari Kirumba kwa kushirikiana na wananchi siku ya Oktoba 21, 2022, baada ya kubainika alienda kwenye mahafali akiwa na panga.

Nyamisi Masinye ni bibi wa Ibrahimu anayedaiwa kuuawa amesema hadi sasa hawajazika mwili huo wakisubiri sheria ichukue mkondo wake kwa waliompiga na kumsababishia kifo mjukuu wake huyo.

"Ninaomba wanisaidie wawakamate waliomuua mjukuu wangu toka tarehe 21 mwezi huu, hata polisi nilivyoenda walisema kwanini wasingempiga hata miguuni? kuliko kumuuwa polisi wapelelezi walisema kwanini wamemuua naomba msaada," amesema Bibi huyo

EATV ikafika hadi shule ya sekondari ya Kirumba ili kutaka kufahamu ukweli kuhusu kijana Ibrahimu anayedaiwa kupigwa akiwa shuleni hapo akasema kumekuwa na matukio ya unyang’anyi katika shule hiyo ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana wanaoishi kuzunguka eneo hilo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad