Baba Amualika Binti yake Aliyemuacha Akiwa na Miaka 2 Kushuhudia Akinyongwa




Binti wa Marekani mwenye umri wa miaka 19 hataweza kushuhudia baba yake akinyongwa, baada ya hakimu kusimamia sheria ya Missouri inayosema umri wa binti huyo ni mdogo kushuhudia tukio hilo.

Kevin Johnson anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa na atanyongwa Jumanne kwa mauaji ya afisa wa polisi mwaka 2005, wakati huo akiwa na umri wa miaka 19.

Aliomba binti yake, Khorry Ramey, ahudhurie na kushuhudia akinyongwa.

Taaisi ya The American Civil Liberties Union iliyowasilisha hoja ya dharura kwa niaba yake, iisema kuwa sheria ya serikali ilikiuka haki zake za kikatiba.


Ilisema kwamba hitaji la umri katika sheria ya Missouri - kumzuia mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 21 kushuhudia kunyongwa - hakukuwa na madhumuni ya usalama.

Johnson, 37, amekuwa gerezani tangu bitni yake, Bi Ramey alipokuwa na umri wa miaka miwili.

Wawili hao walijenga ukaribu mkubwa kupitia kutembelewa gerezani, simu, barua na barua pepe. Na mwezi uliopita tu alimleta mtoto wake mchanga gerezani kukutana na babu yake.


"Nimeumia sana kwamba sitaweza kuwa na baba yangu katika dakika zake za mwisho," Bi Ramey alisema katika taarifa yake, akiongeza kuwa baba yake alifanya kazi kwa bidii ili kujirekebisha gerezani, na kwamba alikuwa akiombea dua ili Gavana wa Missouri kumpa msamaha.

Johnson alipatikana na hatia ya kumpiga risasi afisa wa polisi wa Missouri William McEntee, baba wa watoto watatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad