Winnie Odinga, binti wa kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga, amesema jina lake la familia limemfanya “kunyanyaswa” na “kuteswa” na halikuwa faida ya kisiasa kama wanavyodai baadhi ya wakosoaji.
Winnie Odinga, ambaye anawania kuwa mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alipinga wazo hilo katika kituo cha Citizen TV Kenyakwamba uhusiano wa familia yake ulikuwa nyuma ya uteuzi wake.
Bi Odinga alidai kuwa wakosoaji “hawataki kuangazia ninachoweza kufanya” kwa sababu ya babake ni nani.
Hata hivyo, alikubali kwamba jina la familia yake pia lilikuwa “baraka” ambayo imemruhusu kusafiri ulimwengu na kuelewa jinsi bara la Afrika linaweza kufanya kazi pamoja.
EALA ni chombo cha kutunga sheria cha jumuiya ya kikanda baina ya serikali, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na wanachama wanawakilisha mataifa yao kwa muhula wa miaka mitano.